ILIKUA NI SIKU MBAYA SANA KWA HUYU KIJANA
ZOGO HILI LILIKUTWA NA MPIGA PICHA WETU NA HAKUONA SABABU YA KUACHA KUJUA CHOCHOTE KILICHOMTOKEA KIJANA MTANASHATI ALIEJIZIBA USO. AKIONGEA NA MPIGA PICHA WETU KIJANA HUYU ALIJIKUTA AKICHEZEA KICHAPO KUTOKA KWA WATU HATA ASIOWAJUA, ALISEMA AKIWA MAENEO YA TABATA MAWENZI ALIKUTANA NA MTU ANAEDAIWA ANAMDAI KISHA BAADA YA KUSALIMIANA ALIKAMATWA NA KUMPANDISHA KWENYE DALADALA NA KUMWAMBIA WAELEKEE POLISI KITUO KIDOGO CHA TABATA SHULE. WAKATI WAKITEREMKA KWENYE DALADALA KIJANA AKABADILI MAWAZO NA KUAMUA MUMTORKA MDENI WAKE NA HAPO NDIPO MDAI ALIPOAMUA KUPIGA KELELE ZA MWIZI NA HICHO NDICHO ALICHOKIPATA KIJANA HUYO BAADA YA KUKIMBIA. KIJANA ALIJIKUTA AKIPOKEA KIPIGO HUKU BAADHI WAKIMSAIDIA ASIPIGWE. BAADHI YA WANANCHI WENGINE WALIMGEUKA MDAI KWA KUMSABABISHIA KUPIGWA KIJANA HUYO AMBAE HAKUWA MWIZI. MASIKINI KIJANA ALITAKA KUPOTEZA MAISHA BURE KWA UZEMBE.BAADA YA KUFIKA POLISI MDAI NDIO ALIEBAKI NDANI NA MDAIWA KUACHIWA NA POLISI.
Leave a Comment